• Call Us+255784 519 486
  • Login

IFAHAMU PROGRAM YA BSMART TANZANIA!

Hello Tanzania KARIBU JIUNGE NASI!

BSMART TANZANIA ni Program inayotekelezwa Mikoa yote nchini Tanzania KUJENGA UMAHIRI WA WANAFUNZI KATIKA MASUALA YA SAYANSI, UBUNIFU, TEKNOLOJIA NA VIPAJI na pia KUAMSHA UBUNIFU na KUJENGA UWEZO WA WAJASIRIAMALI WADOGO ikiwa ni pamoja na WASANII kuwawezesha Kushindana kwenye SOKO HURU LA FRIKA na Kuzalisha Fursa za Ajira kwa ajili ya vijana wanaohitimu masomo yao. Program ina vipande sita vinavyoitwa BSMART LEVELS1 to 6. Ninakukaribisha Mjasiriamali, Mwanafunzi na Kijana mwenye Kipaji Ujisajili kuwa sehemu ya Kampeni hii Kabambe iliyozinduliwa tarehe 21.4.2022 Mkoani Mara.

BSMART LEVEL1: Hatua hii tunashirikiana na Bodi za Huduma za Maktaba na Vyombo mbalimbali vya Habari kuhimiza Kampeni ya AMSHA Uwezo wako, AMSHA ubunifu, JENGA  Maarifa. Awamu hii inawahusu Wajasiriamali Wadogo na Wanafunzi ngazi zote kuanzia Vyuo, High School, Sekondari na Msingi. Maktaba zote za Mikoa nchini, Vyuo na Shule zitakazosajiliwa kwenye Programs zitakuwa Vituo vya UBUNIFU kuwezesha Program kuwafikia wahusika wote nchini nzima.

BSMART LEVEL2: Hatua hii Program itajengwa na Kampeni ya ANZISHA, ONYESHA UBUNIFU, ONGEZA Ubora, KUZA Soko lako. Wahusika hapa ni Wajasiriamali Wadogo na Vijana wenye Vipaji waliohitimu Masomo yao ngazi mbalimbali za elimu kuwajengea UWEZO na KUWAWEZESHA kuanzisha miradi ya kijasiriamali ikiwa ni pamoja na Kazi za Sanaa, kuongeza ubora na kukuza masoko yao.

BSMART LEVEL3: Hatua hii tunajikita kuhimiza Matumizi ya Teknolojia ili kuongeza TIJA kwenye Shughuli za Wajasiriamali na Wasanii ili kuwafikia Wateja wengi zaidi na Soko kubwa zaidi. Wahusika hapa ni Wajasiriamali Wadogo na Vijana wenye Vipaji waliohitimu Masomo yao ngazi mbalimbali za elimu.

BSMART LEVEL4: Hatua hii tunajikita kwenye kuwajengea Wajasiriamali Wadogo na Wasanii Uwezo kuboresha na kuimarisha Usimamizi wa Biashara zao na KUONGEZA ajira.

BSMART LEVEL5: Hatua hii tunajikita kujenga USALAMA wa mitaji ya Biashara na kukuza mitaji ya Wajasiriamali Wadogo na Wasanii kwa njia ya Mikopo na Ruzuku.

BSMART LEVEL6: Hatua hii ni GRADUATION ambapo Wajasiriamali Wadogo na Wasanii watajengewa Uwezo wa KUTANUA HIMAYA zao Kuteka FURSA za SOKO HURU la AFRIKA. KARIBU JISAJILI https://bsmartbrands.co.tz/auth/register kuwa mmoja wa Wajasiriamali na vijana wenye Vipaji watakaonufaika na fursa za elimu, mafunzo maalum, ajira, masoko, mitaji na udhamini kupitia mradi huu. Unaweza pia Kutembelea Channel yetu ya YOUTUBE ili KUSUBSCRIBE na Kutazama Vipindi vilivyorushwa: https://youtu.be/1Qq5bTajRJQ   Kwa taarifa zaidi tupigie 0784519486 

JIUNGE NASI!

https://bsmartbrands.co.tz/auth/register

Boniface Ndengo
MRATIBU MRADI WA BSMART TANZANIA