• Call Us+255784 519 486
  • Login

FAHAMU KUHUSU BSMART SCHOOLS

FAHAMU KUHUSU SHULE ZA BSMART NA NJOZI YA BSMART
( BSMART SCHOOLS CUM. BSMART DREAM)

Bsmart Brands Academy tunaamini Kila Mtoto ni Genius katika Eneo fulani, tunaamini Kila Mtoto anacho Kipaji zawadi ya Mwenyezi Mungu ili Kuwa mtu fulani katika Maisha yake. Tunaamini kila mtoto anao Uwezo katika Eneo fulani. Tunaamini Kazi ya Elimu ni Kukuza Uwezo wa Mtoto au Kijana Kufikiri, Kubuni, Kujenga Tabia, Kukuza Uwezo wa mtu na Kumjengea Uwezo wa Kutumia Fursa atakazokutana nazo na pia Uwezo wa Kukabiliana na Changamoto atakazokutana nazo katika Maisha. Tunaamini Teknolojia ni Jambo la Lazima katika Agenda ya Elimu kwa sasa. Tunaamini Malengo ya Kielimu lazima yafungamanishwe na Malengo ya Kiuchumi na Kijamii.

Hivyo BSMART BRANDS tunazo Shule na Programs ambazo Watoto na Vijana watajengewa Uwezo Kitaaluma, Kiteknolojia, Kivipaji, Kiongozi na Kiubunifu. Matarajio ni Kuwapata Vijana Makini ( Smart Kids, Smart Youth) katika Taaluma, Vipaji,  Uongozi, Ubunifu, TEHAMA na Sayansi kwa Matawi yake.

Kwa Primary Darasa la tatu Kila Mtoto anapaswa Kipaji chake kuwa Kimejulikana, Darasa la Tatu Watoto Wataanza Kufundishwa Computer na Wataanza Kufanya Practical za Sayansi.

Kwa Sekondari Program za Taaluma, Vipaji, TEHAMA, Ubunifu, Practical za Kisayansi vinakwenda Sambamba Kuanzia Form One

Mwanafunz wa Shule yoyote Msingi na Sekondari anaweza Kujiunga kuwa Mwanafunzi wa Bsmart Brands Academy na atahudumiwa akiwa shuleni au Siku za Wikiendi au Wakati wa Likizo au Kwa Njia ya Mtandao kwa Kutegemea amechagua njia ipi ya Kupata huduma za Bsmart

Karibu Bsmart, Shiriki Kufanikisha Njozi ya Bsmart  ya Kujenga Kizazi Makini cha Vijana Tanzania ( Smart Kids Generation )

Boniface Ndengo
Mkurugenzi
Bsmart Brands Academy